Thursday, 30 April 2015

Chaweza kuwa takataka kwako lakini kwa mwingine ni faida..

Mifuko ya Cement ambayo yawezekana kuna mwananchi kaitumia kwa kujenga nyumba yake na hatimaye kuitupa, lakini wananchi hawa wa Kasanga,Mkoani Rukwa,wanaitumia mifuko hiyo kama tanga kwenye ngalawa zao wanapokwenda kuvua katika Ziwa Tanganyika na kujipatia kipato. Laweza kuwepo la kujifunza hapo...

Mungu ni wa ajabu angalia hii

Tazama aina hii ya mawe ambayo mojawapo imekaa kama sabuni ya kipande,lakini jiwe jingine likiwa na rangi nyeusi,yote hayo yanapatikana katika Eneo la Kasanga, Mkoani Rukwa. kipo cha kujifunza hapa kwa uumbaji wa Mungu..
Mungu ni wa ajabu ameitengeneza dunia hii na vilivyomo kwa namna yake, hayo mawe yanaonekana kama yamechorwa ngozi ya chui na yako hivyo hivyo, yanapatikana katika Bandari ya Kasanga, Mkoani Rukwa. Kipo hapa cha kujifunza si kwa uumbaji peke yake hata utalii...


Tuesday, 28 April 2015

Usalama wa Abiria na Vyombo vinavyotumia barabara zetu

Usafiri wa Pikipiki ya magurudumu matatau maarufu kama 'Bajaj' umekuwa maarufu sana nchini Tanzania,wakati usalama barabarani ukisisitizwa, Mjini Tunduma,Mbeya, Usafiri huo hubeba abiria sita kwa wakati mmoja,yaani upande wa dereva wanakaa abiria watatu na sehemu ya nyumba wanakaa abiria watatu, kama unavyoona sehemu ya kiti cha dereva kimeongezwa.. Kwa namna hii tutafika kweli na ongezeko hili la ajali?. Nadhani kuna kitu cha kujifunza hapo...

Usafi ni muhimu sana katika utunzaji wa mazingira

Kuna wakati ambao ni muhimu kila mwananchi akatunza mazingira,Miundombinu ya mitaro imejengwa vizuri lakini sisi wenyewe wananchi tunaiharibu mitaro hiyo. mfano ni picha hiyo,mwananchi kamaliza kutumia mifuko ya simenti na akaitupa kwenye mtaro, yawezekana mfuko huo wa simenti ukaenda mpaka mwisho wa mataro huo lakini pia inaweza kusababisha mtaro huo ukaziba. Nadhani kuna kitu cha kujifunza hapo..

Huduma nzuri kwa mteja

Mkoani Rukwa kwa sababu ya baridi,ukishamaliza kula unanawa mikono yako na sabuni,baada ya zoezi hilo, ili mikono yako isipauke unawekewa mafuta ya mgando ili kujipaka mikononi. Huduma kwa mteja ni sehemu ya mafanikio katika biashara yako

Umeshawahi kuona ujenzi wa namna hii...

Waweza kuwa umeona nyumba za kila aina lakini hata nyumba hii ni sehemu ya nyumba nzuri ambazo binadamu wanaishi,wengine hufikiria kuweka madirisha makubwa sana ili kupata hewa lakini mwananchi huyu yeye madirisha sio muhimu sana. Waweza kujifunza kitu......
Ujenzi wa Paa la Nyumba wa aina hii unapatikana Mkoani Rukwa,ukiwa unakwenda kwenye kijiji cha Kipili. Paa hilo la Nyumba limeezekwa kwa nyasi,alafu juu yake vinawekwa vigae. Ninadhani unaweza kujifunza kitu....