Friday, 15 May 2015

Taswira ya maua pembeni mwa Barabara ya Morogoro-Dodoma

Maua yaliyoota pembeni mwa Barabara ya Morogoro-Dodoma kama yalivyokutwa hivi karibuni

Monday, 4 May 2015

Usafiri kutoka kijiji hadi kijiji

Wakati wananchi mbalimbali wakiwa na njia mbalimbali wanazotumia kusafiria kama bajaj,pikipiki(bodaboda),mabasi,hiace(vipanya),wananchi hawa walikutwa wakisafiria gari la mizigo na wamekaa kwenye tela la gari hilo katika barabara ya Itigi-Uvinza kutoka kijiji kimoja kuelekea kijiji kingine. Gari la mizigo laweza kutumika kwa usafiri lakini sina hakika na usalama wa abiria hao.

Ulevi ni Hatari

Kijana ambaye jina lake halikuweza kufahamika akiokota baiskeli yake baada ya kuanguka katikati ya barabara baada ya kuzidiwa na kilevi alichotumia, kama alivyokutwa katika barabara ya Itigi-Uvinza leo mchana. Kijana huyu alipona kwenye ajali ambayo ilikuwa imkute kwani alidondoka na baiskeli yake wakati magari yakipita.

Sunday, 3 May 2015

Mpaka leo karne ya 21 machata yanapigwa

Tanki la maji likiwa limesheheni machata, katika eneo la Nguluka,Uvinza,Mkoani Kigoma

Hata hii nayo ni nyumba ya Ghorofa

Maghorofa sio mjini tu hata vijijini yapo,Uvinza, Kigoma hiyo

Mwanamke wa kitanzania na majukumu

Wanawake hawa wa Kitanzania wakiwa katika shughuli zao za kawaida kama walivyokutwa Nguluka,Uvinza,Mkoani Kigoma

Kijana na wajibu

Add caption
Kijana akiwajibika
Kijana akiwajibika
Watoto wa kike wakijifunza kazi za mikono mapema,Nguluka, Uvinza,Mkoa  wa Kigoma

Makosa ya kimaandishi

Kunaweza kuwa na makosa ya kimaandishi hapo..

Saturday, 2 May 2015

Historia na kumbukumbu

Meli ya MV Liemba ambayo kwa sasa imetimiza miaka 100 tangu kuundwa kwake, ikiwa imepaki katika Bandari ya Kigoma, ambapo picha za hapo chini zinaonyesha bustani iliyotengenezwa kwa mfano wa Meli hii.
Bustani hii ni mfano wa Meli ya MV  Liemba ambayo inafanya safari zake kutoka Kigoma na kupitia katika gati za Kipili, Kasanga mpaka Mpulungu Zambia.  Na mashine nyeupe inayoonekana ni mashine inayotumika kushusha nanga ya meli hiyo, ambayo ilibadilishwa na kuwekwa mpya. Aidha Mnyororo uliozunguka bustani iyo ni mnyororo wa kwanza uliokuwa unashikilia nanga ya meli. Bustani hii iko katika Ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), Mkoani Kigoma.

Ubunifu na Asili

Mawe haya yanasafirishwa kutoka Mkoani Kigoma na kupelekwa Nchini Burundi. Mawe haya husagwa na kupatikana Moram...
Mkungu huu  umeota ndani ya Ziwa Tanganyika, Mkoa wa Kigoma.Mungu kweli ni wa Pekee sana.