Ndoo ya uchafu ikiwa imewekwa kwenye mti ili uchafu utupwe ndani lakini katika hali isiyo ya kawaida kuna uchafu unaonekana chini na sio kwamba ndoo imejaa. Yawezekana wakawa ni kunguru ndo walikuwa wakitafuta chakula katika ndoo hiyo ndo wakasababisha uchafu ukawa chini lakini kuna uwezekano pia kuna binadamu nao wametupa uchafu badala ya ndani ya ndoo hiyo..
Mzee huyu ambaye hakupatikana jina lake alikutwa kwenye Mkutano jijini Tanga,akiwa amevaa picha ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwl Julius Nyerere shingoni mwishoni mwa wiki....
Mwanafunzi huyu ambaye jina lake halikupatikani, alihudhuria katika Mkutano wa Kufunga Wiki ya Mazingira iliyofanyika kitaifa Mkoani Tanga, akiwa na nyumba yake aliyoitengeneza kwa kutumia maboksi.Huyu ni Msanifu majengo mtarajiwa kama kipaji chake kitaendelezwa
Chupa za mafuta zikiwa sokoni kama zilivyokutwa katika barabara ya Bagamoyo-Msata jana jioni. Bei ya mafuta hayo inazingatia viwango vinavyotangazwa na Ewura au wao wanapanga bei wenyewe...
Pikipiki hii kama ilivyokutwa barabara ya Bagamoyo-Msata jana jioni ikiwa imebeba mzigo wa mkaa kuliko uwezo wa chombo hicho, pia hata usalama kwa dreva wa pikipiki hii anapoendesha si wa uhakika kwani hawezi kuona gari inayokuja kutokea nyuma.