Thursday, 30 July 2015

Tumefikia hapa hata kunyonyesha watoto tunaozaa wenyewe ni jambo la kutusisitiza wakati linatakiwa kuwa wajibu

Na. Eliphace Marwa – Maelezo.

Katika kuzingatia na kuboresha afya ya mtoto, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeendelea 
kuwahimiza wanawake kuzingatia utunzaji na ustawishaji wa watoto kwa kuwapa haki ya kunyonya maziwa ya mama.



Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi 
wa Jamii, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Neema Rusibamayila amesema wakati Tanzania inategemea kuungana na mataifa mengine duniani ni vema jamii ikatambua umuhimu wa lishe kwa mtoto.

“Jamii inapaswa kutambua umuhimu wa unyonyeshaji maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto na kuendelea kunyonyeshwa mpaka umri wa miaka miwili au zaidi” alisema Dkt. Neema.

Kwa upande wa mtoto, Dkt. Neema alisema maziwa hayo yana faida nyingi ikiwemo kumpatia 
virutubisho vyote anavyohitaji kwa uwiano sahihi kwa afya na ustawi kwani viini vya 
kingamwili vinavyofanya kazi kama chanjo dhidi ya maradhi humeng’enywa na kufyonzwa 
kirahisi zaidi mwilini tofauti na vyakula vingine.


Aidha aliongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yataenda sanjari na kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio la Innocenti la mwaka 1990ambalo linasisitiza umuhimu wa kulinda, kuendeleza na kusaidia unyonyeshaji na ulishaji bora wa watoto.


Habari kwa hisani ya issamichuzi.blogpsot.com